top of page

Masasisho ya jamii

Kuhusu athari za virusi vya Korona

Kufungwa kwa shule na karantini inatuathiri sote lakini wasiokua raia wa Marekani watakuwa na athari maalum za virasi hii ya korona na athari zake.Majirani duniani aka” Global Neighbours” wamejitolea kuendelea kusaidia waamerika wapya kwa wakati huu mgumu wakishirikiana na jamii, wahisani na wanaojitolea.

Basic_Transparent.png

Kaa Salama//Staying Safe

Staying Safe

Schule//School

School

Gavana wa Dakota Kaskazini,Doug Burgum, ametoa amri kuwa shule zote za Umma zifungwe kuanzia Machi, tarehe ishirini na saba.

 

https://www.health.nd.gov/news/burgum-orders-k-12-schools-close-one-week-effort-slow-spread-covid-19

 

Unaweza pata masasisho haya katika ukurasa wa idara ya afya kwenye mtandao wa kijamii.

SHULE ZA UMMA ZA BISMARCK

 

Shule zote za umma za Bismark zimehamia kufunza wanafunzi kwenye mtandao.

Unaweza pata ya mtoto wako kwenye kiunga kifuatacho

 

https://learnbps.bismarckschools.org/course/view.php?id=8858

 

kisha uchague shule yake na darasa au kiwango chake.

 

SHULE ZA UMMA ZA MANDAN

 

Shule za umma za Mandan zimeanzisha mstari wa msaada kwa familia zisizo na uwezo katika wakati huu mgumu kwa mfano chakula,mavazi,makazi na afya ya kiakili.

Mstari huu unaweza patikana kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili usiku, Jumatatu hadi Ijumaa. Kumbuka ya kwamba mstari huu si wa teknolojia wala uhusiano wa kielimu.

 

Msaada wa Familia: 701-390-9103

Msaada wa kiteknolojia:701-751-6600(ili kumwezesha mwanafunzi wako aweze kupata mafunzo ya mtandao

Iwapo una maswali, wasiliana nasi kwa 701-751-6500

Programu ya wazazi wa Shule za umma za Mandan

 

https://www.youtube.com/watch?v=0h0M3RjZIVA&feature=youtu.be&fbclid=IwAR3dFUAvhvBhlX5D50rPC8HH3MLqwG-CH43MTbDPxMaRyWlvzuR6wzGYvIw

Watoto//Kids

Kids

CHAKULA CHA BURE

 

Mkoba wa kwenda,ambao utakuwa na kishuka na kiamshakinywa za siku ijayo unaweza kuchukuliwa kutoka saa tano unusu asubuhi hadi saa sita unusu adhuhuri kila siku,tangia Jumatatu hadi Ijumaa kwenye mlango wa mbele ama kwenye maegesho ya baadhi ya shule hizi:

BECEP at Richholt,Grimsrud,Moses,Myhre,Will-Moore,Watcher Middle School,Bismarck High,Century High na South Central High School.Mlo pia utapeanwa katika kituo cha gesi cha mzunguko wa Cenex, Lincoln.

Wanafunzi hawataruhusiwa ndani ya mjengo huo kula mlo wao.

 

UTUNZAJI WA WATOTO

 

Kutokana na hali ya shule.kufungwa,wazazi wengi wamo na watoto wao nyumbani wasio na jambo lolote la kufanya.Tafadhali kumbuka watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi na miwili hawafai kuachwa bila usimamizi kwa muda mrefu.

Kama hauna mtunza watoto na unawaacha watoto peke yao nyumbani wasiliana na kanisa lako,majirani ama BGN kwa ushauri.

 

Watoto wanafaa kuwa wakifunzwa n kufanya mazoezi kila siku.

Jaribu kuwatuma watoto nje kwa muda usiopungua dakika thelathini kila siku ili wacheze .Kama kuna barafu hivi kwamba hawawezi kuenda nje kucheza,hapa kuna baadi ya video za mazoezi ambayo wanaweza kufanya wakiwa nyumbani.

YOUTUBE-Jumping Jax

YMCA-Exercises

YOUTUBE-Kids Yoga

 

programu za bure huwa zinasaidia watoto kusoma wakati hawako shuleni:

Lalilo

BrainPop

SmartMusic

Khan Academy

 

Ikiwa watoto wako tayari kuzitazama video za kujiburudisha,chini kuna uchaguzi mzuri.

 

https://pbskids.org/

Lunch Doodles

USAIDIZI//Assistance

Assistance

Habari ifuatayo ni kama kulingana na TaxSlayer.com https://www.taxslayer.com/blog/2020-coronavirus-stimulus-check-how-much-who-qualifies/

 

Uangaliaji wa kichocheo cha virusi vya Korona.

 

Serikali ya Marekani itatuma malipo ya vichocheo kwa njia ya cheki ama kuweka kwenye benki

kwa waamerika wote walipaushuru ili kuwezesha watu kuyakimu mahitaji yao na kuponea virusi vya korona

 

Nani watapata kichocheo hiki?

 

Ili kuweza kushtahiki kwa malipo haya kutoka kwa serikali ya Marekani, sharti uweze kutimiza yafuatayo;

Sharti umelipa Ushuru wako kwa miaka ya 2018,2019 au uwe na fomu ya SSA-1099,kauli ya faida ya usalama wa kijamii au fomu ya RRB-1099 ,kauli ya iliyo sawa na usalama wa kijamii.

 

Sharti uwe umepata chini ya dola elfu sabini na tano,(mtu mzima)

dola mia moja na kumi na mbili elfu na tano(mzazi mmoja ) au dola elfu mia moja na.hamsini kwa walio olewa.

Sharti uwe mwenyeji mgeni(iwapo unayo kadi ya kijani na umelipa ushuru wako au inamtegemea mtu mwingine aliyelipa ushuru,sharti upate cheki.

 

Sharti usidaiwe kuwa unategemea kurudi kwa ushuru wa mtu mwingine.

 

Iwapo haukufaili kurudi kwa ushuru katika mwaka wa elfu mbili kumi na nane,wakati ungali upo wa kufaili kurudi kwa ushuru wa mwaka wa elfu mbili kumi na.Tisa and upate cheki yako ya kichocheo.

 

Je,kichocheo changu kitatumwa wapi?

 

Pesa itawekwa kwenye benki au utumiwe cheki.Waweza amana au ucheki kama kawaida.

Kama haujafaili ushuru wako wa mwaka wa elfu mbili kumi na Tisa, idara ya IRS itaangalia ujumbe wa mwaka wa elfu mbili kumi na nane ili kupata ujumbe ufaao ili waweze kutuma malipo yako.

 

Je, na kama sikufaili ushuru wa miaka ya elfu mbili kumi na nane na kumi na Tisa?

 

Ikiwa haukufaili kwa miaka miwili iliyopita,IRS inapendekeza kuwa ufaili ushuru wa mwaka wa elfu mbili kumi na nane haraka iwezekanavyo ukitumia TaxSlayer.ingia kwenye mtandao kisha uunde akaunti yako alafu uchague kurudi kwa ushuru wa mwaka wa elfu mbili kumi na nane.

 

Kichocheo changu kitawasili lini?

 

Malipo haya yanapaswa kuwasili katika mwezi wa nne kulingana na serikali.Iwapo unapata amana kutoka IRS, basi malipo yako itafika haraka iwezekanavyo kuliko cheki

Na kama nilifaili ushuru na sina kadi ya kijani?

 

Hatujui hayo.

Tutawasiliana baado ya kupokea ujumbe huo.Kwa wakati huu, wasiliana na majirani duniani iwapo huna uwezo wa kununua chakula dawa au kulipa kodi

CHAKULA CHA BURE

bonyeza ili kukuza

 

 

Other local resources: 

www.mvchp.com/resources


https://myfirstlink.org/  or call 2-1-1

FoodMealSites.jpg
adoptablock.jpg

Ukosefu wa Ajira

Unemployment

 

Iwapo umepoteza ajira,kutokana na athari za Korona katika nchi yetu,unaweza faili ili udai malipo ya kukosa ajira kwenye mtandao hapa

 

 

https://www.jobsnd.com/unemployment-individuals/file-claim?fbclid=IwAR2KO4N381-29e5t7oZ-U-v4otz_z-2h3gDcbUqQSYNPiMGb_dF2MSaA29g

 

Iwapo huwezi pata tarakilishi,unaweza kudai kupitia kwa hatua zifuatazo

Piga simu kwa laini ya kazi maalum#701-328-4995 utapata yafuatayo

 

Madai

Tovuti

Kuuliza swali

Sema jina”WEBSITE” kumaanisha tovuti kisha uskize ujumbe wote na mabadiliko yaliyotekelezwa kutokana na virusi vya Korona lakini mwishowe sauti itasema.iwapo ungali na maswali tafadhali usikate simu na mwakilishi atakuwa nawe kwa wakati.Ataweza kukusaidia kufaili kwa simu.

Majirani duniani /Global Neighbours washirika wanaweza kupiga simu kwa 701-595-0135 iwapo unahitaji usaidizi wa lugha unapofaili.

UNEMPLOYMENT_edited.png
English Classes

Darasa la Kiingereza//English class

Tunafahamu ya kwamba familia nyingi humu nchini zimepoteza upatikanaji wa madarasa ya kiingereza kutokana na virusivya Korona katika Adult. learning Centre,Bismarck Public Schools na pia maktaba kutokana na athari za virusi vya Korona.

Majirani Duniani wanathiminia kuandaa programu ya kusoma Kiingereza kwenye mtandao inayoitwa Voxy,iwapo kunao watakaonyesha hamu

Iwapo unafahamu yeyote aliye na.hamu ,tafadhali tutumie barua pepe ili tuweze kujua.

Pia, tunachokikundi cha 'WhatsApp' ili kuweza kuwasiliana na kupitisha ujumbe .

Iwapo we we ni kiongozi wa kikundi chochote cha watu,tafadhali mtumie Leah barua pepe kwa bismarckglobalneighbors@gmail.com ili uweze kuongezwa kwenye kikundi.

 

Hatimaye,kama unafahamu raslimali nyingine ambazo zinaweza kuwa usaidizi kwa jamii,wasiliana nasi ili tuweze kuziongeza kwa ukurasa huu.

Basic_Transparent.png

TUNAWAPENDA,!

bottom of page